Indirimbo Zikundwa Open in the app

#392

Ninakwenda kwetu mbinguni

Coll. des Cantiques

Couplet 1

Ninakwenda kwetu Mbinguni, Nguvu zangu ni zake Bwana, Simo hukumuni wala mautini, Bwana Yesu na asifiwe.

Refrain

Bwana Yesu na asifiwe, Siku zote, njiani pote, Dhambi zangu zote zimeondolewa, Bwana Yesu na asifiwe.

Couplet 2

Ninaye adui ambaye Apenda nipotoke njia, Mimi sikubali, nina Kiongozi, Bwana Yesu na asifiwe.

Refrain

Bwana Yesu na asifiwe, Siku zote, njiani pote, Dhambi zangu zote zimeondolewa, Bwana Yesu na asifiwe.

Couplet 3

Wakihofu wengine wote, Nina nuru rohoni mwangu, Mbele yangu raha na furaha tele, Bwana Yesu na asifiwe.

Refrain

Bwana Yesu na asifiwe, Siku zote, njiani pote, Dhambi zangu zote zimeondolewa, Bwana Yesu na asifiwe.