Indirimbo Zikundwa Open in the app

#296A

Chakutumaini sina

Coll. des Cantiques

Couplet 1

Chakutumaini sina Ila Damu Yake Bwana, Sina wema wa kutosha Dhambi zangu kuziosha.

Refrain

Kwake Yesu nasimama, {Ndiye Mwamba: ni Salama.} x3

Couplet 2

Njia yangu iwe ndefu Yeye hunipa wokovu; Mawimbi yakinipiga Nguvu Zake ndiyo nanga.

Refrain

Kwake Yesu nasimama, {Ndiye Mwamba: ni Salama.} x3

Couplet 3

Damu yake na sadaka Nategemea daima, Yote chini yaki-isha Mwokozi atanitosha

Refrain

Kwake Yesu nasimama, {Ndiye Mwamba: ni Salama.} x3

Couplet 4

Nikiitwa hukumuni, Rohoni nina amani; Nikivikwa haki Yake Sina hofu mbele Yake.

Refrain

Kwake Yesu nasimama, {Ndiye Mwamba: ni Salama.} x3