#240
Wakati wapita mbio
Coll. des Cantiques
Couplet 1
Wakati wapita mbiyo mbiyo nasi Twajongea karibu na kuja kwake Yesu. Karibu na kuja mateso nyingi, Wateule wapita majaribuni.
Refrain
Twajongea karibu na kuja sasa Na karamu ya Arusi ni tayari.
Couplet 2
Bwana Arusi akungoja tu wewe, Njoo mbio nafasi ingaliko ya neema. Wanaingia watu wengi huko, Hujihazimu kuja kwake Yesu Yu.
Refrain
Twajongea karibu na kuja sasa Na karamu ya Arusi ni tayari.
Couplet 3
Hakika karamu ni tayari pale, Shangwe na nyimbo za sifa zitakuwa pale. Wale walio tangulia vile, Watakusanyishwa pamoja na Bwana.
Refrain
Twajongea karibu na kuja sasa Na karamu ya Arusi ni tayari.