Indirimbo Zikundwa Open in the app

#333

Sisi huku si matajiri, kwani miaka yapita

Wokovu

Couplet 1

Sisi huku si matajiri, kwani miaka yapita. Mara nyingi twapata shida, kwani miaka yapita. Tukimwamini Yesu na kumtumikia, tutapata thawabu, kwani miaka yapita.

Refrain

Yapita, yapita, yapita, yapita, tumikieni Mwokozi, kwani miaka yapita.

Couplet 2

Hatutaogopa kitu, kwani miaka yapita. Bali tutafurahi tu, kwani miaka yapita. Dunia ni shida, mashaka na huzuni. Bali tukaze mwendo, kwani miaka yapita.

Refrain

Yapita, yapita, yapita, yapita, tumikieni Mwokozi, kwani miaka yapita.

Couplet 3

Rafiki wanatuacha, kwani miaka yapita. Na safari itaisha, kwani miaka yapita. Tupande mbegu njema, rohoni mwa wenzetu, wengine waokoke, kwani miaka yapita.

Refrain

Yapita, yapita, yapita, yapita, tumikieni Mwokozi, kwani miaka yapita.