Indirimbo Zikundwa Open in the app

#331

Anayeshuhudia kwamba tutafika

Wokovu

Couplet 1

Anayeshuhudia kwamba tutafika Mbingu ni Roho wake Mungu, anayeweka tumaini la kufika Mbingu ni Roho wake Mungu.

Refrain

:/: Tumwombe, tumtafute, Ni wetu Yesu alisema :/:

Couplet 2

Roho yule anafanya njia kati vita kali, kuwaendea ndugu, apungungapo mara tunaanza kuogopa na kujihurumia.

Refrain

:/: Tumwombe, tumtafute, Ni wetu Yesu alisema :/:

Couplet 3

Upendo wako, ndugu uanzapo, kupunguka, ujuwe Roho yule amekwisha kukuacha, pengine mwili wako unaanza kukusonga, tunaye msaidizi.

Refrain

:/: Tumwombe, tumtafute, Ni wetu Yesu alisema :/:

Couplet 4

Tunakuomba, Bwana Yesu, umtume kwetu, msaidizi huyo wa maisha yetu huku. Tunaingia sasa kati vita duniani, wandugu tumuombe Mungu.

Refrain

:/: Tumwombe, tumtafute, Ni wetu Yesu alisema :/: