Indirimbo Zikundwa Open in the app

#272

Nani ni wa Yesu? Amtumikie

Wokovu

Couplet 1

Nani ni wa Yesu? Amtumikie! Atafute watu na kuwahubiri! Nani anataka kujitoa leo, kufuata Yesu katika mateso?

Refrain

Nani ni wa Yesu? Amtumikie! Nani atakaye na amwitikie! Mimi ni wa Yesu, nimtumikie, nitafute watu, kwake warudie!

Couplet 2

Kwa upendo wake tunalazimishwa kutafuta wenye dhambi na makosa. Tunaendelea kuwavuta kwake, hata wanaomba: Mungu tuokoe!

Refrain

Nani ni wa Yesu? Amtumikie! Nani atakaye na amwitikie! Mimi ni wa Yesu, nimtumikie, nitafute watu, kwake warudie!

Couplet 3

Yesu alitununua sisi sote ju’ ya Msalaba na kwa Damu yake. Kwake tumepata raha na uhuru; tunataka sasa kuwa waaminifu!

Refrain

Nani ni wa Yesu? Amtumikie! Nani atakaye na amwitikie! Mimi ni wa Yesu, nimtumikie, nitafute watu, kwake warudie!

Couplet 4

Hata vita ikiongezeka huku tunayo bendera ya kushinda kwetu. Siku ya hatima inakaribia, itaibadili vita iwe shangwe.