#195
Tunasikia leo habari, inawaita watu
Wokovu
Couplet 1
Tunasikia leo habari, inawaita watu wafike; watu wa hapa, watu wa mbali, wote wapate sasa Wokovu!
Couplet 2
Mtu wa dhambi uje upesi, Yesu angoja kukuokoa! Tena kwa nini unachelewa? Leo ni siku ya kuokoka.
Couplet 3
Ulikimbia Yesu Mwokozi aliyekukomboa kwa Damu. Usikimbie mbali zaidi, ila urudi, uje upesi!
Couplet 4
Katika dhambi hutaiona raha halisi, hata kidogo. Yesu mwenyewe atakujaza raha ya kweli ndani ya roho.
Couplet 5
Mtu wa heri katika shida, katika mambo yote ya huku, ni hali ya Mkristo wa kweli, mtu wa heri hata milele.