Indirimbo Zikundwa Open in the app

#187

Tu wavunaji wake Mungu

Wokovu

Couplet 1

Tu wavunaji wake Mungu, kwa neno lake tunakwenda kuvuna ngano zake Yesu alizojinunulia. Kwa shangwe tunaliingiza ghalani mwake vuno lake. Tunamsifu Yesu aliyekomboa vuno lake.

Refrain

Twende kati’ shamba lake, Bwana a’tuita! Vuno linaivya sana, usikie mwito! Siku zetu za mavuno zinatupitia mbio. Siku zetu, siku zetu zinabaki chache.

Couplet 2

Tu wavunaji, twende sasa tukalivune vuno lake, na kwa bidii na imani tukusanye ngano ghali! Katika Pendo kubwa mno anawataka wote, Yesu, na tukiacha suke dogo ataona mara moja.

Refrain

Twende kati’ shamba lake, Bwana a’tuita! Vuno linaivya sana, usikie mwito! Siku zetu za mavuno zinatupitia mbio. Siku zetu, siku zetu zinabaki chache.

Couplet 3

Wakati wetu ni mfupi, a’ita tena, twende mbio! Atujalize uhodari, nguvu ya kuvumilia! Usichelewe bure sasa, watenda kazi ni wachache! E’mvunaji wake Yesu, utumike kwa bidii!

Refrain

Twende kati’ shamba lake, Bwana a’tuita! Vuno linaivya sana, usikie mwito! Siku zetu za mavuno zinatupitia mbio. Siku zetu, siku zetu zinabaki chache.