Indirimbo Zikundwa Open in the app

#184

Nitakwenda mahali pa giza

Wokovu

Couplet 1

Nitakwenda mahali pa giza na dhambi kuhubiri Injili ya nuru, ili watu wasiosikia habari wafahamu upendo wa Yesu.

Refrain

Nitakwenda mahali pa giza na dhambi, hata wote wapate kuona Wokovu.

Couplet 2

Akitaka niende kwa watu wagumu na kuacha rafiki na ndugu, hata wakinitaja: " ’pumbavu " na "bure", nachagua mapenzi ya Yesu.

Refrain

Nitakwenda mahali pa giza na dhambi, hata wote wapate kuona Wokovu.

Couplet 3

Uliyezipoteza dakika na saa kwa tamaa ya mambo ya huku, uamke na uwaokoe wenzako, hata wasipotee kwa dhambi!

Refrain

Nitakwenda mahali pa giza na dhambi, hata wote wapate kuona Wokovu.

Couplet 4

Watu wengi wangali watumwa gizani, wanangoja kupata uhuru, Yesu ananituma, niende upesi kuhubiri maneno ya nuru.

Refrain

Nitakwenda mahali pa giza na dhambi, hata wote wapate kuona Wokovu.