#167
Ninajua rafiki Mwema, anitunza
Wokovu
Couplet 1
Ninajua Rafiki Mwema, anitunza sana kila siku. Ayaponya majeraha na machozi ayafuta. Jina lake ni Yesu Kristo.
Refrain
Najua Rafiki Mwema, na yeye ajaa ne’ma. Nikiomba asikia, afariji nikilia. Ndiye Yesu, na si mwingine.
Couplet 2
Nimepata Rafiki Mwema, afariji na kunipa raha. Nikitegemea yeye sitahofu maadui; na rafiki ni Yesu Kristo.
Refrain
Najua Rafiki Mwema, na yeye ajaa ne’ma. Nikiomba asikia, afariji nikilia. Ndiye Yesu, na si mwingine.
Couplet 3
Nifikapo mtoni pale paitwapo "kufa" na "mtego", sitafadhaika hapo, Yesu atakuwa nami; ni Rafiki mkubwa mno.
Refrain
Najua Rafiki Mwema, na yeye ajaa ne’ma. Nikiomba asikia, afariji nikilia. Ndiye Yesu, na si mwingine.
Couplet 4
Pwani nzuri ya huko juu nifikapo kwa Neema kuu, nitaimba kwa kinubi, nitasifu Yesu sana kwa upendo na urafiki.