Indirimbo Zikundwa Open in the app

#150

Nataka kupokea baraka yake Mungu

Wokovu

Couplet 1

Nataka kupokea baraka yake Mungu, nataka kubatizwa kwa Roho ’takatifu. Ju’ ya ahadi yake napumzika sana, aliahidi mimi kupata Roho yake.

Refrain

Sawa na bahari, sawa na bahari ni Neema yake anileteayo. Anayenijaliza, anayeniponyesha, ni Mwokozi wangu. Asifiwe sana!

Couplet 2

Kanisa lake Mungu linaipata mvua, vijito vya baraka vinamiminwa sasa. Furaha ya uzima ni kubwa kati yetu. Tuimbe haleluya! Tumshukuru Yesu!

Refrain

Sawa na bahari, sawa na bahari ni Neema yake anileteayo. Anayenijaliza, anayeniponyesha, ni Mwokozi wangu. Asifiwe sana!

Couplet 3

Mawimbi ya Wokovu yanatujia sasa. E’ Mungu, tunaomba: Ujaze sisi sote! Watakatifu wako watakasike sana! Tuimbe haleluya! Tumshukuru Yesu!

Refrain

Sawa na bahari, sawa na bahari ni Neema yake anileteayo. Anayenijaliza, anayeniponyesha, ni Mwokozi wangu. Asifiwe sana!

Couplet 4

Mawimbi ya Wokovu yaliyofika kwetu, E’ Mungu, uyatume ulimwenguni mwote, maelfu kati watu wapate kuokoka, waimbe haleluya, wamshukuru Yesu!

Refrain

Sawa na bahari, sawa na bahari ni Neema yake anileteayo. Anayenijaliza, anayeniponyesha, ni Mwokozi wangu. Asifiwe sana!