#125
Haleluya! Nafurahi, ninaimba
Wokovu
Couplet 1
Haleluya! Nafurahi, ninaimba kila siku sifa zake Mungu wangu, aliyeniweka huru. Haleluya! Bwana Yesu aliniokoa kweli! Haleluya! Mimi wake, yeye ni Mwokozi wangu!
Couplet 2
Heri! Nilieokoka kwa Neema yake kubwa ninataka kumsifu Mungu na Wokovu wake. Wakinung’unika wote, sitawafuata wao; nitasifu Mungu wangu siku zote na milele.
Couplet 3
Kama ndege waimbavyo asubuhi bustanini, Na sauti ya mawingu ivumavyo baharini, hivyo nitamshukuru Bwana wangu kwa furaha. Roho yangu itaimba: Haleluya! Sifu Mungu!
Couplet 4
Haleluya! Furahini mbele yake Mungu wetu! Na watakatifu wote, mwimbieni jina lake! Malaika wote pia, ... ...msifuni Bwana Mungu! Mbingu zote zitajibu: Haleluya, Haleluya!