#110
Mwamba uliopasuka
Wokovu
Couplet 1
Mwamba uliopasuka, ndani yako nijifiche! Maji yale, Damu ile itokayo mbavu zako, iwe dawa ya kuponya roho yangu na ubaya!
Couplet 2
Kazi za mikono yangu, haziwezi kukomboa. Hata ningelia sana na kutenda kazi nyingi, singeweza kuokoka, peke yako u Mwokozi.
Couplet 3
Ndani yangu sina kitu, naushika Msalaba. Uchi mimi, univike! Sina nguvu, ’nichukue! Ni mchafu, unioshe! Wewe u Mwokozi wangu.
Couplet 4
Kwa maisha yangu yote hata nitatoa roho, hata saa ya kuitwa mbele ya Mfalme wangu, Mwamba uliopasuka, nijifiche ndani yako!