Indirimbo Zikundwa Open in the app

#90

Yesu, Yesu, jina kubwa

Wokovu

Couplet 1

Yesu, Yesu, jina kubwa, nyimbo zao malaika! :/: Limekuwa ndani yangu mto wa furaha bora:/:

Couplet 2

Jina lake kama nyota, linanionyesha njia. :/: Katika jaribu, shida, na usiku duniani. :/:

Couplet 3

Ni mikono ya upendo yenye kunikumbatia. :/: Hapo najificha vema, kama chombo bandarini.:/:

Couplet 4

Jina hilo liwe kwangu, wimbo wa safari yangu! :/: Niletewe wema nalo, toka nchi nzuri juu! :/: