Indirimbo Zikundwa Open in the app

#73

Najua njia moja yakufika Mbinguni

Wokovu

Couplet 1

Najua njia moja yakufika Mbinguni, ingawa ikipita katika majaribu, lakini iendako mjini huko juu, :/: Na njia hiyo Yesu. :/:

Couplet 2

Najua na amani iliyo ya milele, huwezi kuipewa kwa fedha na dhahabu; ni tunu ya rehema iliyotoka Baba. :/: Amani hiyo Yesu. :/:

Couplet 3

Najua nguvu moja yakuniponya roho, initiayo raha, amani na faraja, inanilinda vema na nguo yangu safi, :/: Na nguvu hiyo Yesu:/:

Couplet 4

Najua na kifiko Mbinguni huko juu, na siku ni karibu kita’poonekana. Yafa’kukaza mwendo, kupiga mbio sana! :/: Kifiko ni Mbinguni. :/: