Indirimbo Zikundwa Open in the app

#66

Wakristo wa nchi zote

Wokovu

Couplet 1

Wakristo wa nchi zote watakusanyika huko Mbinguni kwa Yesu, mezani pake, kati’ ufalme wake; kuona uzuri wake, kujazwa Neema yake. Wataimba huko ju’ milele na milele.

Refrain

Watoka bahari zote, watoka katika shida, watoka milima, watoka mabonde kufika kwa Mungu Baba, kuvikwa mavazi safi, kuona Mwokozi wao, yeye ali’wafilia ju’ ya Msalaba.

Couplet 2

Watakusanyika wengi walikotoka huku. Mateso na kufa, shida na giza hawata’ona kamwe. Ya kale hayatakuwa, lo! yote ni mapya huko! Itakuwa raha tu pamoja na faraja.

Refrain

Watoka bahari zote, watoka katika shida, watoka milima, watoka mabonde kufika kwa Mungu Baba, kuvikwa mavazi safi, kuona Mwokozi wao, yeye ali’wafilia ju’ ya Msalaba.

Couplet 3

Tazama mlango huko uliokufunguliwa, na kuna mahali Yesu aita: « Njoo nyumbani kwangu wenzetu waliofika wanatungojea huko, malaika wanaimba kukukaribisha.

Refrain

Watoka bahari zote, watoka katika shida, watoka milima, watoka mabonde kufika kwa Mungu Baba, kuvikwa mavazi safi, kuona Mwokozi wao, yeye ali’wafilia ju’ ya Msalaba.