Indirimbo Zikundwa Open in the app

#57

Yesu, uliyekufa kwa ajili yangu

Wokovu

Couplet 1

Yesu, uliyekufa kwa ajili yangu, ninajitoa kwako, niwe mali yako! Bwana, nivute kwako, nifaamishe pendo, niwe dhabihu hai katika shukrani!

Couplet 2

Yesu, nafika kwako, kao la rehema; Bwana, nitie nguvu kwa Neema yako! Niuchukue tena kwa radhi Msalaba, ni’tumikie wewe, Mkombozi wangu!

Couplet 3

Bwana, uniumbie moyo haki, safi, kwako niishi tena hata kufa kwangu! Niwatafute wenye dhambi na udhaifu, niwapeleke kwako, Bwana wa upendo!

Couplet 4

Vyote ninavyo huku nimepewa nawe, ukivitaka, Bwana, uvitwae vyote! Nina urithi wangu kwako Mbinguni juu, nitakuona huko kwa furaha kuu!