#175
Mashujaa wa imani
Umuco
Couplet 1
Mashujaa wa Imani, wa kati wa mbere, walisimamia kweli kazi ya Mungu Baba, walisinziya wote, wanangoja taji zao, kwa ajiri yao wote, tumepata Wokovu kweli ni sifa kwa Mungu Baba ./.Oo, haleluya!./.
Refrain
Hao wote watafufukia Uzima wa milele, na waliyo na hekima watangaa kama mwanga wa anga, na waongozao wengi katika njia ya haki, watangaa kama nyota ./.Milele, kwa furaha ya milele, na milele./.
Couplet 2
Mashujaa wa imani wamepigania kweli, kazi ya Mungu Baba injili yake Bwana, walijitowa zaidi katika hali yoyote kwa ajili yao wote, tumepata Wokovu kweli, ni sifa kwa Mungu Baba ./.Oo, haleluya!./.
Refrain
Hao wote watafufukia Uzima wa milele, na waliyo na hekima watangaa kama mwanga wa anga, na waongozao wengi katika njia ya haki, watangaa kama nyota ./.Milele, kwa furaha ya milele, na milele./.
Couplet 3
Mashujaa wa imani mitume na manabii, wainjilisti wachungaji, waalimu na wazee, watoa huduma wote, na waonyaji pia, wasimamizi na waaskofu, na wengine wote ni sifa kwa Mungu Baba ./.Oo, haleluya!./.
Refrain
Hao wote watafufukia Uzima wa milele, na waliyo na hekima watangaa kama mwanga wa anga, na waongozao wengi katika njia ya haki, watangaa kama nyota ./.Milele, kwa furaha ya milele, na milele./.
Couplet 4
Na sisi siku izi, tujitoe kwa zaidi, tuseme habari njema, katika wapotevu, wahubiri muhubiri, wahuduma muhudumie, kwa hali yoyote tumutumikie Bwana.tutavikwa taji huko ./.Oo, haleluya!./.