#335
Kila siku bwana
Umuco 1
Couplet 1
Kila siku, Bwana, kazi yako, Ni kazi inayopita fahamu, Aki1i haijuwi kazi hiyo, Mwanadamu naye haijuwi, Isipokuwa aliyefunuliwa
Refrain
{Na nyuma ya Kazi hiyo, Patakuwa kupewa malipo, Waliyohudumu ipasavyo, Watapewa kitani cha Uzima, Uzima... Uzima wa milele.} x2
Couplet 2
Bwana Mungu ulipoanza kazi, Uliwaita watumishi wako, Ukawapa na lile Neno lako, Roho wako wa kuwaongoza, Wapate kuwa na ujasiri wote.
Refrain
{Na nyuma ya Kazi hiyo, Patakuwa kupewa malipo, Waliyohudumu ipasavyo, Watapewa kitani cha Uzima, Uzima... Uzima wa milele.} x2
Couplet 3
Na Eliya mtumishi wako, Ulimuita katika kazi hiyo, Akawindwa ili apate kufa, Akitafutwa na yule Ahabu, Lakini Bwana ulimshindia.
Refrain
{Na nyuma ya Kazi hiyo, Patakuwa kupewa malipo, Waliyohudumu ipasavyo, Watapewa kitani cha Uzima, Uzima... Uzima wa milele.} x2
Couplet 4
Watumishi wako, Bwana Mungu, Mara nyingi huona matatizo, Kwa sababu kazi hiyo ni ngumu, Na We’ Baba unawawezesha, Ukiwapa kudumu katika Neno.
Refrain
{Na nyuma ya Kazi hiyo, Patakuwa kupewa malipo, Waliyohudumu ipasavyo, Watapewa kitani cha Uzima, Uzima... Uzima wa milele.} x2
Couplet 5
Jipeni moyo taifa la Mungu, Maana Bwana amefurahia, Kutupa ufalme kwa Neema, Siku ya ukombozi inakuja, Na sasa, Bwana Yesu yu mlangoni.