#79
Tafuteni ufalme wake
Umuco 1
Couplet 1
T’afuteni ufalme wake Bwana, Na nguvu za ufalme, Tafuteni uzima wake Bwana, Vingine vitatufuata.
Refrain
Ufalmeni mwa Baba, Kunajaa upendo, Ufalmeni mwa Baba kunajaa amani, Ufalmeni mwa Baba kunajaa furaha, {Ni sifa kwa Bwana wetu.} x2
Couplet 2
Tafuteni vizuri vya ufalme, Na utajiri usiooza, Tafuteni vazi la arusi, Ishara zitatufuata.
Refrain
Ufalmeni mwa Baba, Kunajaa upendo, Ufalmeni mwa Baba kunajaa amani, Ufalmeni mwa Baba kunajaa furaha, {Ni sifa kwa Bwana wetu.} x2
Couplet 3
Tafuteni uso wake Bwana, Na utukufu wake, Tafuteni upendo wake Bwana, Karama zitatufuata.
Refrain
Ufalmeni mwa Baba, Kunajaa upendo, Ufalmeni mwa Baba kunajaa amani, Ufalmeni mwa Baba kunajaa furaha, {Ni sifa kwa Bwana wetu.} x2
Couplet 4
Tuzifuate nyayo zake Bwana, Na bidii alikua nayo, Tuenende kama alivyoenenda, Tutaurithi ufalme.
Refrain
Ufalmeni mwa Baba, Kunajaa upendo, Ufalmeni mwa Baba kunajaa amani, Ufalmeni mwa Baba kunajaa furaha, {Ni sifa kwa Bwana wetu.} x2
Couplet 5
Tukiwa na uzima wake Bwana, Karama zitatumika, Tukiwa na nguvu zake Bwana, Vyote tutavipata.