Indirimbo Zikundwa Open in the app

#15

Mimi niko na matumaini

Umuco 1

Couplet 1

Mimi niko na matumaini, Yangu yote kwako Bwana. Nina unyonge wa mwili wangu, Niwezeshe kuushinda.

Refrain

Uwe kwangu e’ Bwana wangu, Nami niwe mahali pako, Maana Wewe ni mwamba wangu, Wewe ndiye rafiki yangu, Kinywa changu kitajalishwa, Sifa zako... heshima zako.

Couplet 2

Niwezeshe kwa neema yako, Kwa upendo na huruma, Inamisha sikio lako, Kwangu mimi ewe Bwana.

Refrain

Uwe kwangu e’ Bwana wangu, Nami niwe mahali pako, Maana Wewe ni mwamba wangu, Wewe ndiye rafiki yangu, Kinywa changu kitajalishwa, Sifa zako... heshima zako.

Couplet 3

Nikumbushe kwa siku zote, Pendo lako ewe Bwana, Niongoze kwa Neno lako, Liwe taa kwangu mimi.

Refrain

Uwe kwangu e’ Bwana wangu, Nami niwe mahali pako, Maana Wewe ni mwamba wangu, Wewe ndiye rafiki yangu, Kinywa changu kitajalishwa, Sifa zako... heshima zako.

Couplet 4

Unitiye imani mwangu, Niamini ahadi zako, Niongoze kwa Neno lako, Niwashinde adui zangu.