Indirimbo Zikundwa Open in the app

#161

Usiku uingiapo

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Usiku uingiapo, umwaze Mungu Mkuu, aendeshaye dunia kwa mwendo mtulivu.

Couplet 2

Kwa nini wahangaika usiku namchana? Umtwishe huzuni yako aliyekuumba.

Couplet 3

Kwake haujapunguka uwezo na msaada. Atayatimiza yote aliyoyaanza.

Couplet 4

Ukamwachie kutenda atakalo kwako! Kwa hiyo ulale raha na kufurahiwa.