#94
Siku ya Mbingu kujawa na sifa
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Siku ya Mbinguni kujawa na sifa, Dhambi zilizidi duniani; Yesu akaja azaliwe mtu, Awe na watu ulimwenguni.
Refrain
Alinipenda, alinifia, Ameondoa na dhambi zangu; Alifufuka nipewe haki, Yuaja tena Mwokozi wangu.
Couplet 2
Na siku moja walikwenda naye, Wakamkaza Msalabani; Aliumia, aliaibishwa, Ili atuokoe dhambini.
Refrain
Alinipenda, alinifia, Ameondoa na dhambi zangu; Alifufuka nipewe haki, Yuaja tena Mwokozi wangu.
Couplet 3
Siku hiyo wakamlaza chini Kaburini alipumzika; Matumaini yetu wenye dhambi, Ni Mwokozi, kwake twaokoka.
Refrain
Alinipenda, alinifia, Ameondoa na dhambi zangu; Alifufuka nipewe haki, Yuaja tena Mwokozi wangu.
Couplet 4
Kaburi likashindwa kumshika; Jiwe likatoka mlangoni, Alifufuka kwa kushinda kwake, Naye yuko milele Mbinguni.
Refrain
Alinipenda, alinifia, Ameondoa na dhambi zangu; Alifufuka nipewe haki, Yuaja tena Mwokozi wangu.
Couplet 5
Siku moja atatujia tena; Utukufu wake tutaona; Atawaleta na wapenzi wetu; Mwokozi: wangu, tutaonana.