Indirimbo Zikundwa Open in the app

#5

Jina lake Yesu tamu

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Jina lake Yesu tamu; Tukilisikia Hutupoza, tena hamu Hutuondolea.

Couplet 2

Roho iliyoumia Kwalo hutibika, Chakula, njaani pia; Raha, tukichoka.

Couplet 3

Jina hili ni msingi, Ngao, ngome, mwamba, Kwa hili napata wingi, Kwangu ni akiba.

Couplet 4

Yesu, Mchunga, Rafiki Mwalimu, Kuhani, Mwanzo, Mwisho, Njia, Haki, Uzima kifoni.

Couplet 5

Moyo wangu hauwezi, Kukusifu kweli, Ila sifa zangu hizi, Bwana zikubali.

Couplet 6

Na utakaponiita, Kuja kwako Bwana, Huko kwako sitaacha Kukusifu sana.