Indirimbo Zikundwa Open in the app

#3

Hata ndimi elfu

Tenzi za Rohoni

Couplet 1

Hata ndimi elfu elfu, Hazitoshi kweli Bwana Yesu kumsifu, Kwa zake fadhili.

Couplet 2

Yesu, jina liwezalo Kufukuza hofu; Lanifurahisha hilo, Lanipa Wokovu.

Couplet 3

Jina hilo ni uzima; Ni afya amani; Laleta habari njema; Twalipiwa deni.

Couplet 4

Yesu huvunja mapingu Ya dhambi moyoni; Msamaha, tena nguvu, Twapata rohoni.

Couplet 5

Kwa sauti yake vile Wafu hufufuka Wakafurahi milele, Pasipo mashaka.

Couplet 6

Ewe Yesu wangu Bwana, Uwezo nipewe, Kuhubiri kote sana, Wote wakujue.