#1
Mwokozi Umeokoa
Tenzi za Rohoni
Couplet 1
Mwokozi umeokoa, Nimekuwa wako wewe. Damu imenisafisha; Sifa kwa mwana Kondoo.
Refrain
Utukufu, Halleluya! Sifa kwa Mwana Kondoo! Damu imenisafisha, Utukufu kwa Yesu!
Couplet 2
Nilijitahidi sana Ila sikupata raha; Bali kwa kumtegemea Nilipata Baraka.
Refrain
Utukufu, Halleluya! Sifa kwa Mwana Kondoo! Damu imenisafisha, Utukufu kwa Yesu!
Couplet 3
Daima namwegemea Damu ikifanya kazi, Nikioga kwa chemichemi Itokayo Mwokozi.
Refrain
Utukufu, Halleluya! Sifa kwa Mwana Kondoo! Damu imenisafisha, Utukufu kwa Yesu!
Couplet 4
Sasa nimewekwa wakfu; Nitaishi kwako wewe: Fahari nashuhudia Ya Wokovu wa bure.
Refrain
Utukufu, Halleluya! Sifa kwa Mwana Kondoo! Damu imenisafisha, Utukufu kwa Yesu!
Couplet 5
Nasimama kwake Yesu, Ameponya roho yangu; Ameniondoa dhambi, Anifanye mzima.
Refrain
Utukufu, Halleluya! Sifa kwa Mwana Kondoo! Damu imenisafisha, Utukufu kwa Yesu!
Couplet 6
Nilikuwa kifungoni, Niliteswa na dhambi, Nilifungwa minyororo Yesu akanifungua.
Refrain
Utukufu, Halleluya! Sifa kwa Mwana Kondoo! Damu imenisafisha, Utukufu kwa Yesu!
Couplet 7
Sifa, ameninunua! Sifa, nguvu za Wokovu! Sifa, Bwana huhifadhi! Sifa zake milele.