#327
Siku mateso yatakapokwisha
Nyimbo za Mungu
Couplet 1
Siku mateso yatakapokwisha, Kule Mbinguni nitakapofika, Kuwa na Yesu Mwokozi karibu, Hii ni furaha kupita kipimo.
Refrain
Hii ni furaha, na utukufu, Na utukufu, na utukufu; Kuwa na Yesu Mwokozi karibu, Hii ni furaha kupita kipimo.
Couplet 2
Kwa maana nimeamini Mwokozi, Nitamusifu daima Mbinguni; Kumutazama kwa macho karibu, Hii ni furaha kupita kipimo.
Refrain
Hii ni furaha, na utukufu, Na utukufu, na utukufu; Kuwa na Yesu Mwokozi karibu, Hii ni furaha kupita kipimo.
Couplet 3
Ndugu wananingojea Mbinguni, Tutafurahi pamoja milele; Yesu akinipokea karibu, Hii ni furaha kupita kipimo.
Refrain
Hii ni furaha, na utukufu, Na utukufu, na utukufu; Kuwa na Yesu Mwokozi karibu, Hii ni furaha kupita kipimo.