Indirimbo Zikundwa Open in the app

#317

Ninakuomba, Yesu

Nyimbo za Mungu

Couplet 1

Ninakuomba, Yesu, ndiwe Kondoo wa Mungu, Wewe Mwokozi, Sasa Unisikie, vile Unisafishe, Unitakase niwe wako pekee.

Couplet 2

Kwa Neema yako kubwa unipe mimi nguvu Kwa kazi yako; Ulinikufilia, hivi mapendo kwake Yawake ndani yangu kama moto.

Couplet 3

Dunia ina giza, mateso, na huzuni, Uniongoze; Ee, ufukuze giza, mateso, na huzuni, Usiniache kukufuata mbali.

Couplet 4

Siku ya kufa kwangu, ninapokwenda ngambo, Sitaogopa; Mikono ya mapendo itanibeba kwako, Niwe pamoja nawe kwa milele.