#289
Mwokozi Anaishi
Nyimbo za Mungu
Couplet 1
Mwokozi Anaishi, ni hapa duniani; Ni neno la hakika, ni neno la furaha. Ananihurumia, ananifurahisha, Na anakaa karibu sikuzote.
Refrain
Mwokozi ni hai, ni hai kwa milele, Anatembea nami kwa safari yangu yote; Mwokozi ni hai, tayari kuokoa, Na ninajua namna gani? Ni hai moyoni mwangu.
Couplet 2
Ananipenda kweli na kunichunga sana, Na hata ninachoka, nadumu kumufuata; Katika mambo yote Mwokozi ndiye Bwana, Kufika siku atakaponitwaa.
Refrain
Mwokozi ni hai, ni hai kwa milele, Anatembea nami kwa safari yangu yote; Mwokozi ni hai, tayari kuokoa, Na ninajua namna gani? Ni hai moyoni mwangu.
Couplet 3
Nasi Wakristo wote, tusifu sikuzote, Tuimbe Haleluya kwa Kristo na Mufalme; Anapokea wote wanaofika kwake, Hakuna anayependa kama yeye.