Indirimbo Zikundwa Open in the app

#257

Siku nyingine taabu ‘takwisha

Nyimbo za Mungu

Couplet 1

Siku nyingine taabu ‘takwisha, Vile huzuni na majaribu; Siku nyingine tutapumzika, Saa ya kurudi kwa Bwana Yesu.

Refrain

Siku nyingine Yesu Mwokozi Atatokea kutukamata; Tutasikia Sauti yake Akituita sisi na wewe.

Couplet 2

Unasumbuka? utafurahi utasahau kila huzuni. Utafanana naye Mwokozi, na utamwona uso kwa uso.

Refrain

Siku nyingine Yesu Mwokozi Atatokea kutukamata; Tutasikia Sauti yake Akituita sisi na wewe.

Couplet 3

Tutakutana naye kwa hewa, kisha furaha itatimia; Tutaonana na ndugu zetu, tutatukuza Kristo milele.

Refrain

Siku nyingine Yesu Mwokozi Atatokea kutukamata; Tutasikia Sauti yake Akituita sisi na wewe.