#231
Nimeahidi, Yesu, nitakutumikia
Nyimbo za Mungu
Couplet 1
Nimeahidi, Yesu, nitakutumikia; Usiniache kamwe, Rafiki yangu mwema; Sitaogopa taabu pamoja nawe, Yesu, Na sitahangaika, nikiongwa nawe.
Couplet 2
Ee Bwana, unichunge katika majaribu Yanayonizunguka kwa kunitamanisha; Adui ni karibu, ni hata ndani yangu; Ee Bwana, karibia na chunga nafsi yangu.
Couplet 3
Umeahidi, Yesu, kwa watumishi wako Kukaa pamoja nawe katika utukufu; Nimeahidi, Yesu, nitakutumikia Unipatishe nguvu nifuate nyuma yako.