Indirimbo Zikundwa Open in the app

#229

Ninakushukuru, Bwana

Nyimbo za Mungu

Couplet 1

Ninakushukuru, Bwana, kwani uliniokoa; Vile ulinisafisha niwe chombo chako safi.

Refrain

Chombo chako, Bwana Yesu, Niko mikononi mwako; Unijaze, utumie, kila siku, kila saa.

Couplet 2

Mimi chombo ‘tupu, Bwana, unijaze na baraka; Hivi maji ya uzima yatatoka ndani yangu.

Refrain

Chombo chako, Bwana Yesu, Niko mikononi mwako; Unijaze, utumie, kila siku, kila saa.

Couplet 3

Sina nguvu ila yako, ndiyo Roho yako, Mungu; Unijaze na uwezo niwe mushuhuda wako.

Refrain

Chombo chako, Bwana Yesu, Niko mikononi mwako; Unijaze, utumie, kila siku, kila saa.

Couplet 4

Mimi chombo cha udongo, utukuzwe ndani yangu; Ulininunua Bwana, niwe kweli mali yako.

Refrain

Chombo chako, Bwana Yesu, Niko mikononi mwako; Unijaze, utumie, kila siku, kila saa.