Indirimbo Zikundwa Open in the app

#221

Yesu, unapita ndugu

Nyimbo za Mungu

Couplet 1

Yesu, unapita ndugu na rafiki za dunia; Kwa maisha yangu yote nikufuate tu karibu.

Refrain

Nikufuate wewe, Yesu, nikufuate wewe, Yesu, Kwa maisha yangu yote nikufuate tu karibu.

Couplet 2

Sitamani mali tena wala sifa na heshima. Kitu hiki ninataka, nikufuate tu karibu.

Refrain

Nikufuate wewe, Yesu, nikufuate wewe, Yesu, Kwa maisha yangu yote nikufuate tu karibu.

Couplet 3

Hata unaniongoza kwa mateso na huzuni, Nitafika siku moja kupumzika kwako, Yesu.

Refrain

Nikufuate wewe, Yesu, nikufuate wewe, Yesu, Kwa maisha yangu yote nikufuate tu karibu.