Indirimbo Zikundwa Open in the app

#212

Askari wa Mwokozi

Nyimbo za Mungu

Couplet 1

Askari wa Mwokozi mimi na mufuata wake, Sitaogopa kutangaza Jina la Mwokozi.

Couplet 2

Sitaogopa majaribu na kupata taabu Katika vita na makosa kwa ajili yake.

Couplet 3

Nitapigana na adui na uwezo wake; Dunia inamuchukia Yesu Bwana wangu.

Couplet 4

Ee Bwana, niwe muhodari, niwe mwaminifu, Nibebe taabu na uchungu kwa Neema yako.