Indirimbo Zikundwa Open in the app

#198

Ee Mwokozi, Unilinde

Nyimbo za Mungu

Couplet 1

Ee Mwokozi, Unilinde na Uniongoze kweli, Njia ni matata sana, bila Wewe nitaanguka.

Refrain

Bwana Yesu, Uni’ngoze kwa upole, Nikufuate duniani kila siku, kila saa.

Couplet 2

Wewe ndiwe kimbilio kwa wakati wa zoruba, Nawe siogopi kitu, kwako tumaini langu.

Refrain

Bwana Yesu, Uni’ngoze kwa upole, Nikufuate duniani kila siku, kila saa.

Couplet 3

Kisha siku ya mauti utanifikisha kwako, Nitazame uso wako, na machozi yatakwisha.

Refrain

Bwana Yesu, Uni’ngoze kwa upole, Nikufuate duniani kila siku, kila saa.