Indirimbo Zikundwa Open in the app

#178

Navutwa kwake Yesu

Nyimbo za Mungu

Couplet 1

Navutwa kwake Yesu na ninamufurahia, Uzuri wake unapita vyote vya dunia; Siwezi kuupima kweli kwa mawazo yangu, Uzuri wake unazidi kuwa bora kwangu.

Refrain

Siwezi kueleza uzuri wake huko, Lakini nitaufahamu wote kule Mbingu.

Couplet 2

Mapendo ya ajabu kubwa nayasifu sana, Yakanivuta kwa upole, nije kwake Bwana; Yakanitoa mimi katika unyonge wangu, Mapendo yake yanazidi kuwa bora kwangu.

Refrain

Siwezi kueleza Mapendo wake huko, Lakini nitayafahamu yote kule Mbingu.

Couplet 3

Wokovu wake wa ajabu usifiwe sana, Uliondoa woga, ukanipa utulivu; Napenda Yesu aliyechukua zambi zangu, Wokovu wake unazidi kuwa bora kwangu.

Refrain

Siwezi kueleza Wokovu wake huko, Lakini nitaufahamu wote kule Mbingu.