#166
Jua la roho ni wewe
Nyimbo za Mungu
Couplet 1
Jua la roho ni wewe, Mwokozi, Giza haliko pahali ulipo; Wingu la zambi lisifiche Uso wa Bwana machoni mwangu.
Couplet 2
Hata kwa saa ya kulala usiku Sitaogopa, wewe ni karibu. Nitapumzika kwa salama Kwani unanifunza daima.
Couplet 3
Saa ya muchana unanishindisha, Nitaanguka usiponichunga, Uache nuru ya Mbinguni Kunionyesha njia ya haki.
Couplet 4
Uwe karibu nami saa ya kufa, Uniongoze kwa bonde la giza Unifikishe kwako juu, Nione uso wako Mbinguni.