Indirimbo Zikundwa Open in the app

#159

Yesu unayenipenda

Nyimbo za Mungu

Couplet 1

Yesu unayenipenda, leo nijifiche kwako; Zambi kama mvua kubwa zimetaka kunishinda. Ee Mwokozi, unifiche, unitwae niwe kwako, Niokoke kwa mabaya na nisiwe mbali nawe.

Couplet 2

Wewe tu ni kimbilio, hapa ni matata mengi; Ninakuhitaji sana, Ee usiniache pekee. Mimi ninakuamini, wewe Musaidizi wangu; Chini ya mabawa yako ninachungwa na salama.

Couplet 3

Yote ninayoitaji ninapata kwako, Bwana; Roho inapolegea, unisimamishe tena. Wewe mwenye haki pia, mimi mwenye zambi kubwa; Wewe pekee unaweza kusafisha moyo kweli.

Couplet 4

Neema nyingi iko kwako kufunika zambi zangu; Unitwae, unichunge, unilinde hata mwisho. Hivi nikukaribie, unishike kwa mikono: Nikujue wewe pekee, hapa chini, kule juu.