#155
Nani anayeninyanyua?
Nyimbo za Mungu
Couplet 1
Nani anayeninyanyua? Ni Yesu Kristo; Na anayenipigania? Ni Yesu Kristo. O Yesu ninakuamini, wewe tu utanishibisha, Kwami silala ya kushinda ni Yesu Kristo.
Couplet 2
Mwenye kunifikisha Mbingu ni Yesu Kristo; Mwenye kunipa shangwe kubwa ni Yesu Kristo. Na hata katika mateso na masumbuko, majaribu, Kwami taraja na furaha ni Yesu Kristo.
Couplet 3
Nani aliyeniokoa? Ni Yesu Kristo; Nani anayefaa kwangu? Ni Yesu Kristo. Bado kidogo nitakwenda kule Kwa nyumba yake Baba. Na nitaishi kwa milele na Yesu Kristo.