Indirimbo Zikundwa Open in the app

#152

Niwe karibu nawe, Ee Mungu wangu

Nyimbo za Mungu

Couplet 1

Niwe karibu nawe, Ee Mungu wangu, Hata katika taabu niwe karibu; Huu wimbo wangu, Bwana: Niwe karibu nawe, Niwe karibu nawe, Ee Mungu wangu.

Couplet 2

Ninasafiri hapa, sitakawia; Giza ni duniani, raha haiko; Hata ni hivi, Bwana, niwe karibu nawe, Niwe karibu nawe, Ee Mungu wangu.

Couplet 3

Hata mateso mengi yananipata, Nitakumbuka hili, unarehema, Na yatanikokota niwe karibu nawe, Niwe karibu nawe, Ee Mungu wangu.

Couplet 4

Saa nitakapokwenda kwako Mbinguni, Nitasahau taabu ya duniani; Ungali wimbo wangu niwe karibu nawe, Niwe karibu nawe, Ee Mungu wangu.