#148
Pahali pote ninapokwenda
Nyimbo za Mungu
Couplet 1
Pahali pote ninapokwenda, Ama kwa jua, ama kwa giza, Yesu Mwokozi aliahidi hatanipungukia daima.
Refrain
Nuru ya Mbingu, Nuru ya Mbingu, Ninatembea sasa kwa Nuru; Haleluya Ninamusifu na shangwe kubwa, Yesu ni wangu.
Couplet 2
Wakati taabu inapokuja, Yesu hawezi kunisahau; Aliahidi neno la kweli, atanichunga hata milele.
Refrain
Nuru ya Mbingu, Nuru ya Mbingu, Ninatembea sasa kwa Nuru; Haleluya Ninamusifu na shangwe kubwa, Yesu ni wangu.
Couplet 3
Ninamusifu kwa nuru yake inayoniongoza kwa njia; Nikitembea kando ya Yesu, sitapotea hata kidogo.
Refrain
Nuru ya Mbingu, Nuru ya Mbingu, Ninatembea sasa kwa Nuru; Haleluya Ninamusifu na shangwe kubwa, Yesu ni wangu.
Couplet 4
Katika njia kwenda Mbinguni Niendelee ndani ya nuru, Ninamwimbia nyimbo za sifa Kumushukuru kwa Pendo lake.