Indirimbo Zikundwa Open in the app

#103

Siwezi mimi kufahamu sana

Nyimbo za Mungu

Couplet 1

Siwezi mimi kufahamu sana Neema yake Mungu kwangu; Zamani nilikuwa mukosaji, sasa amenisamehe.

Refrain

Ninajua Mwokozi wangu Anayeweza kulinda sana Uriti kwami Mbinguni hata siku yake Bwana.

Couplet 2

Siwezi mimi kufahamu sana namna alivyonivuta; Niliamini Neno lake kweli, ninaona raha tele.

Refrain

Ninajua Mwokozi wangu Anayeweza kulinda sana Uriti kwami Mbinguni hata siku yake Bwana.

Couplet 3

Siwezi mimi kufahamu kazi Roho anayoifanya, Anayeweza kufundisha mutu kuamini Yesu Kristo.

Refrain

Ninajua Mwokozi wangu Anayeweza kulinda sana Uriti kwami Mbinguni hata siku yake Bwana.

Couplet 4

Sijui mimi siku zangu tena kutembea duniani; Na labda nitaona taabu na mateso na huzuni nyingi.

Refrain

Ninajua Mwokozi wangu Anayeweza kulinda sana Uriti kwami Mbinguni hata siku yake Bwana.

Couplet 5

Sijui mimi kama siku moja nitaona kufa huko; Ao kwa haraka nitabadilika Bwana atakapokuja.