Indirimbo Zikundwa Open in the app

#67

Tunazikwa kwa kaburi la Mwokozi

Nyimbo za Mungu

Couplet 1

Tunazikwa kwa kaburi la Mwokozi Yesu Bwana; Mungu anatuhesabu kuwa wafu kwa makosa.

Couplet 2

Kufa na hukumu vile haziwezi kutugusa; Bwana alibeba yote, nguvu yao amemaliza.

Couplet 3

Yesu alifufuliwa toka wafu, yeye kwanza; Nasi tumeumbwa tena, sisi ni wahuru sasa.

Couplet 4

Ubatizo tunapata, sura ya mauti yake; Nasi tunafufuka naye, ndani yake tunakaa.

Couplet 5

Tunangoja ukombozi wa miili yetu vile; Atatugeuza pia kufanana naye Yesu.

Couplet 6

Bwana, sasa tunataka kushiriki haya yako; Mungu atatupokea, kwani tuko ndani yako.