Indirimbo Zikundwa Open in the app

#51

Jina la Pendo kubwa

Nyimbo za Mungu

Couplet 1

Jina la Pendo kubwa, Yesu Mwokozi, Linalopita yote Yesu Mwokozi; Sisi hatuna kitu kukupendeza, Mungu. Sharti utupe yote, Yesu Mwokozi.

Couplet 2

Ulifanyika mwili, Yesu Mwokozi, Na ulitoa damu, Yesu Mwokozi Ulilishuhudia pendo lililo kubwa Kuliko pendo lote, Yesu Mwokozi.

Couplet 3

Na kwako tuna haki, Yesu Mwokozi, Makimbilio letu, Yesu Mwokozi; Hatuna woga mwingi wa taabu na huzuni, Kwako tunafichama, Yesu Mwokozi.

Couplet 4

Utarudia tena, Yesu Mwokozi, Kwa kutimiza raha, Yesu Mwokozi; Bwana, tutakuona, halafu tutakuwa Sawa nawe milele, Yesu Mwokozi.