#49
Ee Baba, nitakuwa kama Yesu
Nyimbo za Mungu
Couplet 1
Ee Baba, nitakuwa kama Yesu, Baraka ile alinipatia Ni mushangao na ajabu pia, Kwa sura yake atanigeuza.
Couplet 2
Ee Bwana Yesu, nani kama wewe Alinipenda hata nitazameMilele utukufu wako, Kristo, Mimi zawabu ya mateso yako?
Couplet 3
Mapendo yako hayakustarehe Mbele ya kubariki wana wako; Yanashiriki vitu vyote nasi, Hata uriti wako, Bwana Yesu,
Couplet 4
Wapenzi wako wote kwa milele Kwa utukufu watakusanyika, Na kwa furaha watakuzunguka, Kukuabudu na kukutukuza.