Indirimbo Zikundwa Open in the app

#33

Yesu, unitazamishe Musalaba wako

Nyimbo za Mungu

Couplet 1

Yesu, unitazamishe Musalaba wako, Nisikusahau wewe na mauti yako.

Refrain

Musalaba wako, Bwana, ni taraja yangu Hata nitakapokwenda kupumzika kwako.

Couplet 2

Nilitetemeka pale, mimi mwenye zambi; Kwa mapendo na rehema ulinipokea.

Refrain

Musalaba wako, Bwana, ni taraja yangu Hata nitakapokwenda kupumzika kwako.

Couplet 3

Yesu, unilinde huko, unifahamishe; Jinsi ulivyochukua zambi zangu zote.

Refrain

Musalaba wako, Bwana, ni taraja yangu Hata nitakapokwenda kupumzika kwako.

Couplet 4

Nitangoja na taraja na imani vile Hata nitakapokwenda kwako kwa milele.

Refrain

Musalaba wako, Bwana, ni taraja yangu Hata nitakapokwenda kupumzika kwako.