Indirimbo Zikundwa Open in the app

#26

Yesu, Mwanzo wa uzima

Nyimbo za Mungu

Couplet 1

Yesu, Mwanzo wa uzima, tunaishi kwako, Bwana; Ulishinda Diabolo, haya, woga, vile kufa. Ulipita kwa mateso kwa kuturudisha kwako; {Mashukuru elfu elfu yawe kwako kwa milele.} x2

Couplet 2

Bwana Yesu, ulipata fimbo na kuzarauliwa; Wewe Bwana wa wabwana, walikuvalisha miiba; Wewe ulituokoa kwa vifungo vya makosa; {Mashukuru elfu elfu kwako, Bwana na Mwokozi.} x2

Couplet 3

Walitia haya nyingi juu yako, Ee Mwokozi; Ulitubebea yote kwa kuleta ukombozi. Kwa uchungu wako, Bwana, tunaweza kuokoka; {Mashukuru elfu elfu kwako, Bwana na Mwokozi.} x2

Couplet 4

Sifa ya mioyo yetu tunakupa, Bwana Yesu; Kwa mateso na mauti uliyopokea yote. Ulidumu kwa huzuni kwa kutupatia raha; {kwa milele tutaimba mashukuru kwako, Bwana.} x2