#261
Ukingoni mwa yordani
Izindi
Couplet 1
Ukingoni mwa Yordani ninaangalia Bara nzuri ya Kaanani, ninayotamani.
Refrain
Tutakaa pamoja na Yesu, katika pwani yenye raha; Tutaimba wimbo wa Musa na Kondoo, milele hata milele.
Couplet 2
Bara ile ina nuru, nuru ya milele; Kristo, Jua, hutawala, hufukuza giza.
Refrain
Tutakaa pamoja na Yesu, katika pwani yenye raha; Tutaimba wimbo wa Musa na Kondoo, milele hata milele.
Couplet 3
Nitapafikia lini penye kubarikiwa, penye Ufalme wa Baba. Na kumwona Uso?
Refrain
Tutakaa pamoja na Yesu, katika pwani yenye raha; Tutaimba wimbo wa Musa na Kondoo, milele hata milele.
Couplet 4
Furaha yangu rohoni ni kuchukuliwa; Siyaogopi mawimbi katika Yordani.