Indirimbo Zikundwa Open in the app

#257

Msikie bwana anawaita

Izindi

Couplet 1

Msikie Bwana anawaita wenye kulemewa wasumbukao, njoo kwake Yesu Awapumzishe, kila shida zote Atachukua.

Refrain

Uje leo akupumzishe, Nira yake Bwana ni nyepesi mno. Yeye mnyenyekevu, mpole kabisa, mwepesi mzigo, njoo Kwake leo.

Couplet 2

Umechoka sana rohoni mwako, Unayo mashaka mengi moyoni? Uje kwake Yesu na shida zote leo akuita Akupumzishe.

Refrain

Uje leo akupumzishe, Nira yake Bwana ni nyepesi mno. Yeye mnyenyekevu, mpole kabisa, mwepesi mzigo, njoo Kwake leo.

Couplet 3

Umepotea dhambini kabisa Hukumu milele utaingia, lakini Mchungaji ndiye Mwokozi, Atakuokoa ukija kwake

Refrain

Uje leo akupumzishe, Nira yake Bwana ni nyepesi mno. Yeye mnyenyekevu, mpole kabisa, mwepesi mzigo, njoo Kwake leo.

Couplet 4

Mbona je! hushindi majaribuni, utapewa nguvu njoo kwake Yesu. Kwa uwezo Wake utashinda tu Roho Mtakatifu Akupumzishe.