#243
Zitakapokwisha taabu zote
Izindi
Couplet 1
Zitakapokwisha taabu zote; Takuwa Mbinguni na Bwana wetu; Nitaruhusiwa kuketi naye; Furaha yangu itakamilika.
Refrain
Furaha kuketi naye, Baraka ya kweli ni kwangu; Nitaruhusiwa kuketi naye; Furaha kwangu milele.
Couplet 2
Nitakapomwona Mwokozi kule; Aliyenifilia Msalabani; Kumwimbia mwenye Neema huyo; Furaha yangu itakamilika.
Refrain
Furaha kuketi naye, Baraka ya kweli ni kwangu; Nitaruhusiwa kuketi naye; Furaha kwangu milele.
Couplet 3
Milele kukaa nyumbani mwake; Pamoja na wote Watakatifu; Kumsifu na kumtukuza Yesu; Furaha yangu itakamilika.
Refrain
Furaha kuketi naye, Baraka ya kweli ni kwangu; Nitaruhusiwa kuketi naye; Furaha kwangu milele.